Sehemu ya sasa:
Somo Je, mtu anaingiaje katika Uislamu?
Mtu anaingia katika Uislamu anapotamka shahada mbili pamoja na kujua maana yake huku akiwa na yakini nazo, na kutii mambo yote yanayohitajiwa nazo.
Na shahada mbili ni:
Wakati mtu anapoingia katika Uislamu ni wakati mkubwa zaidi wa maisha yake, na ni kuzaliwa kwake kwa kweli. Baada ya hapo, anajua sababu ya kuwepo kwake katika maisha haya. Na ni jambo linaloruhusiwa kisheria anapoingia katika dini kwamba aoge na afikishe maji vyema kwenye mwili wake wote. Kama vile alivyotakasa mambo ya ndani yake kutokana na ushirikina na dhambi, inapendekezwa kwake kuitakasa sehemu yake ya nje kwa kuoga kwa maji.
Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimuamuru Swahaba mmoja - ambaye alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa Waarabu, – alipotaka kusilimu kwamba aoge. (Al-Bayhaqi 837)
Toba
Toba ni kurudi kwa Mwenyezi Mungu. Kila anayeacha uasi na ukafiri wake na kumrudia Mwenyezi Mungu huku akiwa mkweli moyoni mwake, basi atakuwa ametubu kwa Mwenyezi Mungu.
Masharti ya toba kuwa sahihi:
Hatua za kukaa imara katika toba
Ni nini kinachfaa baada ya toba?
Mtu akitubia na kurudi kwa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu husamehe madhambi yote, hata yawe makubwa kiasi gani, kwani rehema yake, aliyetakasika imeenea kila kitu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." (Az-Zumar: 53)
Basi Muislamu hutoka baada ya toba ya kweli na iliyo sahihi hali ya kuwa hana dhambi yoyote. Bali Mwenyezi Mungu Mtukufu huwalipa wakweli, wanyenyekevu, wanaojuta sawasawa kwa malipo makubwa zaidi. Yeye huwabadilishia maovu yao yakawa matendo mema, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Isipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao, Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu." (Al-Furqan: 70)
Yeyote aliye katika hali hii, basi anapaswa zaidi kudumisha toba hiyo na kutoa kila kitu kilicho ghali na cha thamani kubwa ili asije akaanguka tena katika mitego ya Shetani inayompelekea kurudi nyuma tena.
Yule ambaye upendo wake Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio upendo mkubwa zaidi kwake, na akawa anawapenda wengineo kwa kiasi cha ukaribu wao kwa Mwenyezi Mungu na usahihi wa dini yao na Uislamu wao, na akawa anakuchukia kurejea katika ukafiri aliokuwamo, na ushirikina na upotofu, kama vile anavyochukia kuchomwa na Moto, basi atapata kwamba imani ina utamu na raha moyoni mwake kutokana na kuliwazwa na kutulia anakohisi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kufurahia sheria ya Mwenyezi Mungu na neema zake juu yake kwa kumuongoa. Kama alivyosema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: “Matatu, yule ambaye hayo yatakuwa ndani yake basi atapata utamu wa Imani: Yule ambaye Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio vipenzi zaidi kwake kuliko kisichokuwa wawili hao, na yule anayempenda mja, na hampendi ila tu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na yule anayechukia kurudi katika ukafiri kama anavyochukia kutupwa ndani ya Moto.” (Bukhari 21, Muslim 43)
Kushikamana na dini na subira juu ya udhia ndani yake:
Mwenye kumiliki hazina ya thamani kubwa huwania sana katika kuilinda ili isichukuliwe na mikono ya waharibifu na wezi, na huilinda kutokana na kila chenye kuiathiri. Uislamu ndiyo neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu humpa mwanadamu. Uislamu siyo mwelekeo wa kifikira tu au hobi anayofanya mtu wakati wowote anapotaka. Bali ni dini inayotawala maisha yote ya mtu, pamoja na harakati zake na kutulia kwake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwambia Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akimuamrisha kushikamana kwa nguvu na Uislamu na Qur-ani na kwamba asiachilie mbali chochote miongoni mwa hayo; kwa sababu yeye yuko kwenye njia iliyonyooka: "Basi wewe yashike vilivyo yale yaliyofunuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye njia iliyonyooka." (Az-Zukhruf: 43)
Na Muislamu hatakiwi kuhuzunika akipatwa na aina fulani ya msiba baada ya kusilimu, kwani hiyo ni desturi ya Mwenyezi Mungu katika kuwajaribu waja wake. Kwa sababu watu ambao ni bora kuliko sisi walijaribiwa kwa misiba mzito, lakini wakasubiri na wakafanya juhudi. Misiba iliwajia Manabii wa Mwenyezi Mungu kutoka kwa jamaa zao hata kabla ya watu wa mbali, lakini hawakudhoofishwa na yale yaliyowasibu katika njia ya Mwenyezi Mungu, na hawakubadilika wala kugeuka. Kwa sababu majaribu ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili kuonyesha ukweli wa imani ya Muislamu na nguvu ya yakini yake. Basi ni na awe kwa daraja sawa na mtihani huo, na ashikamane vilivyo na dini hii, na amuombe Mwenyezi Mungu kama Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie alivyokuwa akiomba dua sana akisema: “Ewe Mwenye kubadilisha mioyo, uimarishe moyo wangu juu ya dini yako.” (Tirmidhi 2140)