Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Mwanamke na miito ya kisasa

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu itikadi muhimu zaidi, misingi na miito ya kisasa inayoathiri masuala ya wanawake.

  • Kuonyesha uadilifu wa Sheria na hekima yake katika kushughulikia masuala ya wanawake.
  • Kuelezea misingi na fikira muhimu zaidi za kisasa zinazoathiri masuala ya wanawake.
  • Kubainisha baadhi ya kasoro za miito iliyopotoka katika kushughulikia masuala ya wanawake.

Katika nyakati za kale na katika ustaarabu mwingi wa kale, wanawake hawakuwa na sura yoyote ya kibinadamu yenye heshima. Walikuwa wamepuuzwa na kutohesabiwa kuwa chochote. Bali hawakuwa na haki au ustahiki wowote, na walikuwa wakiuzwa na kununuliwa bila kujali ubinadamu wao. Pia walikuwa wakionekana kuwa duni kuliko wanaume.

Njia hii iliendelea kudharau wanawake katika ustaarabu na tamaduni tofauti tofauti hadi hivi karibuni. Ingawa ulimwengu wa Magharibi, kwa mfano, baadaye ulianza hatua ya mabadiliko na ukombozi kutoka kwa ukandamizaji wa utawala na dhuluma ya kanisa. Lakini mabadiliko haya hayakuwafikia wanawake na masuala yao isipokuwa kwa kuchelewa.

Fikira hii potofu katika mtazamo wake kuhusu wanawake ilikuwa ikiungwa mkono na pande mbili kuu:

1. Upande wa kifalsafa

Wanafalsafa katika karne za kale waliwadharau wanawake, wakawadunisha na hawakuwaona kwamba wana hadhi yoyote wala haki. Miongoni mwa wanafalsafa hawa ni Sokrates, Plato, na Aristoteli.

2. Upande wa kidini

Katika Uhindu, mwanamke hana haki ya kurithi kutoka kwa wazazi wake. Yule ambaye mumewe anakufa, inalazimu kumchoma mwanamke huyu pamoja na mumewe, kwa sababu ni bora zaidi kwake asiishi baada yake! Ama kwa Wayahudi na Wakristo, wanawake walikuwa na hadhi ya chini mno, na walikuwa wakishutumiwa kwamba wao ndio chanzo cha uovu, uasherati na dhambi, na walichukuliwa kama najisi. Mawazo haya yalitokana na vitabu vyao vilivyopotoshwa, na kutokana na mikutano ya kidini iliyofanyika, na ilikuwa ikuungwa mkono na mamlaka ya makasisi na kanisa.

Katika enzi ya kisasa, itikadi, fikira na nadharia kadhaa zimeibuka ambazo zimeathiri - na zinaendelea kushawishi - fikira, mitazamo na tabia za jamii nyingi kuhusu wanawake.

1. Usasa na baada ya usasa

Usasa humfanya mwanadamu kuwa kitovu cha ulimwengu, na unasisitiza kumpa uhuru wake mbali na Ufunuo, na kwamba kwa akili yake anaweza kujitolea mwenyewe tafsiri mbalimbali kuhusiana na yeye mwenyewe, mazingira yake na ulimwengu. Na fikira nyingi, mitazamo, na uchambuzi uliofuata baada ya hapo ulitokana na usasa huu.

2. Kutumia akili tu

Ni kuinuliwa hadhi ya akili na vipimo vyake; kwa msingi kwamba mwanadamu ndiye kitovu cha ulimwengu.

3. Uhuru na ubinafsi

Inamaanisha kusisitiza haki ya binadamu ya kuamua hatima ya mambo yake ya kiraia kwa njia ambayo anaiona kuwa ndiyo inafaa kwake.

4. Nadharia ya Darwini

Ni nadharia ambayo inazungumza juu ya asili ya mwanadamu na maendeleo yake kwa mamilioni ya miaka hadi akawa katika hali ya sasa.

5. Ukombozi wa wanawake

Fikira ya kuwakomboa wanawake iliibuka barani Ulaya, ambapo wanawake walikuwa wakiteseka kutokana na ukandamizaji na dhuluma, kwa hivyo wakainua kauli mbiu za uhuru na ukombozi kutoka kwa mambo yaliyorithiwa yaliyokwisha pitwa na wakati. Huko, wanawake walipokea haki nyingi za kibinadamu, kijamii, kisiasa na kiuchumi, lakini madai haya hayakuwa na kidhibiti cha kidini au cha kithamani cha kuyapangilia vyema. Kwa hivyo wakageukia miito ya kujikomboa kutoka kwa dini na maadili, siyo kujikomboa kutoka kwa udhalimu na ukandamizaji. Haya yote yakafunikwa chini ya madai ya kujikomboa kutoka kwa utawala au udhibiti wa kiume.

Usekula na suala la kuwakomboa wanawake

Miongoni mwa fikira na miito ambayo imehusishwa na maana ya ukombozi wa wanawake ni kutenganisha dini na mambo yote ya maisha, na kutumia usekula kama mfumo wa maisha. Maana hii inahusishwa na usekula kwa njia ya kulinginia ukombozi wa wanawake kutoka kwa kila kitu kinachozuia matarajio yake, haswa udhibiti wa kidini na mafundisho yake.

6. Usekula

Hili linamaanisha kutenganisha kati ya dini na kila kitu kinachohusiana na kuendesha maisha, na kuanzia kwa mwanadamu mwenyewe kama rejea ya shughuli za kibinadamu katika nyanja mbalimbali; kisiasa, kiuchumi, kijamii na nyinginezo.

7. Usawa wa kijinsia

Wito huu unategemea juu ya msingi wa kuweka usawa kati ya wanaume na wanawake katika haki ya elimu, kazi, haki za kiraia na kisiasa na mengineyo, na kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake. Hata hivyo, madai ya kuweka usawa katika haki yalitoka katika muktadha wake wa kimsingi, na yakawa hayajali tofauti kati ya wanaume na wanawake, na yakawa wito wa kusawazisha kati ya viwili vilivyo tofauti.

8. Ufeministi

Fikira inayolingania ukombozi wa wanawake na usawa wa kijinsia inaitwa "fikira ya kifeministi." Harakati mbalimbali zimeibuka kutoka kwa fikira hii ambazo zinafanya shughuli nyingi za kiakili, kisiasa, kijamii na nyinginezo. Fikira hii ya kifeministi, pamoja na shughuli zake mbalimbali, vimejaribu kuimarisha fikira na mazoea mengi katika jamii.

Misingi ya fikira ya kifeministi

١
Uhuru kamili ambao umesimama juu ya fikira ya jamii inayotegemea mtu binafsi na siyo familia.
٢
Kutegemea dhana ya jinsia katika kuelezea uhusiano kati ya jinsia mbili hizi, na kuondoa dhana ya mwanamume na mwanamke.
٣
Umiliki wa mwanamke wa mwili wake, na haki yake kamili ya kufanya chochote anachotaka bila vizuizi vyovyote wala udhibiti.
٤
Kuondoa jukumu la baba katika familia, kwa kukataa mfumo wa utawala wa baba.
٥
Kulingania - kupitia baadhi ya mikondo ya kifeministi - ushoga, kuruhusu kuavya mimba, na fikira ambazo huharibu silika ya mwanadamu, maadili yanayohusiana na ulimwengu na itikadi.

Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW)

Mashirika ya haki za wanawake na taasisi za wanawake zilifanya juhudi za kupata msaada wa kisiasa, kupitia mataifa mbalimbali kuidhinisha mkataba wa kimataifa uliopitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1979, ili kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake, ambao ni Mkataba wa Kuondoa Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW).

Undani wa Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW).

Mkataba huu unategemea juu ya usawa kamili na ulinganifu kati ya wanaume na wanawake katika nyanja zote; kisiasa, kiuchumi, kijamii, michezo, kisheria na nyanja zinginezo. Hii ni kanuni isiyo sahihi, yenye kuhalifu sheria za kimungu, yenye kupingana na maana dhahiri ya Kitabu na Sunna na kile kilichopendekezwa na akili timamu, na kukubaliwa na silika zilizonyooka. Ama ukiukaji wake Kitabu, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Na mwanamume si sawa na mwanamke." [Al-Imran: 36] Na kauli yake, "Wanaume ni wasimamizi madhubuti wa wanawake." [An-Nisaa: 34] Na kauli yake Mwenye Nguvu, Mtukufu, "Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao." [Al-Baqarah: 228] Na kuhusu ukiukaji wake wa Sunna, alisema Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “Nyote ni wachungaji, na nyote mnawajibika kwa walio chini ya uchungaji wenu. Mwanamume ni mchungaji katika familia yake, na ataulizwa juu ya wale walio chini ya uchungaji wake. Na mwanamke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe, na ataulizwa juu ya wale walio chini ya uchungaji wake.” (Al-Bukhari 893, Muslim 1829). Na ama kuhusu kupingana kwake na kile kilichothibiti katika fahamu sahihi, basi hilo si katika mambo yanayohitaji ufafanuzi mwingi, kwa sababu ni wazi kwamba tofauti katika muundo wa kimwili na kisaikolojia lazima zisababishe tofauti katika uwezo na kazi za maisha. Kwa hivyo, kufikia usawa kamili na ulinganifu ni kinyume na maumbile asili ya kiume na ya kike.

Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) na kuleta kwake uhasama kati ya wanaume na wanawake.

Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) na harakati za kifeministi, zinaonyesha kwamba uhusiano ulioko kati ya wanaume na wanawake ni kama uhusiano wa ushindani na migogoro ya kihistoria, ambayo wanataka kumaliza. Njia yake ya kufikia hilo ni kusawazisha kikamilifu kati ya wanaume na wanawake, wakidai kuwa kuwapa wanaume ubora wowote wa ziada ni kwa gharama ya wanawake. Huu ni mtazamo mwembamba mno; kwani uhusiano ulioko kati ya mwanamume na mwanamke ni uhusiano wa kukamilishana na ushirikiano, siyo ushindani na uhasama. Kila mmoja wao ana jukumu lake na kazi yake, kwa maelewano na kukamilishana, ili kuimarisha maisha, kujuana, upendo, huruma, na utunzaji wa kila jinsia. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Enyi watu, hakika Sisi tumewaumba kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumewajaalia kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua zaidi, Mwenye habari zote." [Al-Hujurat: 13] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na katika Ishara zake ni kuwa amewaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaotafakari." Kutofautiana kwa majukumu ya kimaisha kunalazimu kuwepo utofauti katika haki na majukumu bila ya dhuluma au ukandamizaji. Kwa hivyo, kila jukumu la ziada, linakabiliana na haki zaidi, na huu ndio uadilifu.

Je, Sheria inataka kuwe na usawa kati ya wanaume na wanawake?

Sheria imeweka usawa kati ya wanawake na wanaume katika asili ya kibinadamu na hadhi ya viumbe, katika uwajibikaji na kubeba amana, katika adhabu za kidunia na za kiakhera, katika kila mmoja wao kustahiki haki yake, na katika kutekeleza ibada na kuhukumu kwa Sheria na kuwa na maadili mema. Kwa kuongezea, Sheria inaweka ubaguzi mzuri kati yao kwa sababu ya tofauti zao katika muundo wa kimwili na kisaikolojia. Wanawake hawatakiwi kufanya jihadi kwa sababu ya udhaifu wa muundo wao. Pia hawaswali wala kufunga saumu wakati wa hedhi na baada ya kujifungua. Pia hawalazimiki kutoa pesa za matumizi ya nyumbani, hata akiwa ni tajiri. Kwa upande mwingine, Sheria iliweka jihadi kwa wanaume, na kuwawajibisha kuwapa matumizi wanawake na watoto wao, jukumu ambalo wanaadhibiwa juu yake ikiwa watakataa au watafalifanya vibaya. Kwa sababu ya majukumu haya ya ziada wamepewa haki zaidi. Huu ndio uadilifu wenyewe.

Uadilifu wa Sheria katika Urithi

Hakuna dhuluma yoyote kwa wanawake katika urithi katika sheria za Kiislamu. Kwani wakati mwingine yeye huchukua chini ya fungu la wanaume, na wakati mwingine anachukua fungu sawa naye, na wakati mwingine anachukua zaidi ya fungu lao, na wakati mwingine yeye hurithi, nao wanaume hawarithi. Hayo yote ni kwa sababu ya hekima ambayo Mwenyezi Mungu ndiye anaijua zaidi, na hayo yameelezewa katika vitabu vya wanazuoni.

Miongoni mwa yenye kuonyesha heshimu ambayo Sheria imempa mwanamke.

Mwanamke amehifadhiwa na kuheshimiwa katika sheria ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, "Mwenye kutenda uovu, hatalipwa isipokuwa sawa na huo uovu wake. Na anayetenda wema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi, waruzukiwe humo bila ya hesabu." [Ghafir: 40] Naye Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie amesema, “Hakika wanawake ni washirika wa wanaume.” (Tirmidhi 113). Mlezi wa mwanamke (baba au mume) anawajibishwa kumpa makazi na matumizi, naye hatwikwi kutoa matumizi hata dinari moja - isipokuwa tu kama yeye mwenyewe atatoa kwa hiari yake - hata kama atakuwa tajiri namna gani. Pia anastahiki kuwa na mali sawa na mwanamume, na hakuna mtu yeyoye aliye na ulezi wa kimali juu yake, si baba wala mume. Pia mwanamke ana haki ya kujifanyia mambo mwenyewe kama vile kuuza, kununua, kukodisha (kuajiri), kufanya ushirikiano na wengine, kuweka rehani, kukiri, kudhamini, kupatanisha na mikataba mingineyo na majukumu.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani