Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Mavazi ya mwanamke wa Kiislamu

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu mambo kadhaa muhimu yanayohusiana na mavazi ya mwanamke wa Kiislamu.

  • Kujua neema ya Mwenyezi Mungu kwa watu kwa kuwapa mavazi na mapambo.
  • Kujua baadhi ya hukumu za sheria ya Kiislamu zinazohusiana na mavazi ya wanawake.
  • Kujua masharti ambayo lazima yatimizwe katika hijab ya kisheria.
  • Kujua mipaka ya kile ambacho mwanamke Mwislamu anaweza kudhihirishia sampuli mbalimbali za watu.

Neema ya mavazi

Kuvaa mavazi ni neema kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambayo kwayo mwanadamu hujisitiri mwili wake na kuulinda dhidi ya joto, baridi, na mambo mengineyo, na ni mapambo na uzuri. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Enyi wanadamu, tumewateremshia vazi la kuficha tupu zenu, na mapambo. Na vazi la uchamungu ndilo bora. Hayo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu ili wapate kukumbuka." [Al-A'raf: 26] Kuna mavazi ambayo ni muhimu kwa kila mwanamume na mwanamke, ambayo ni yale yenye kufunika uchi. Na kuna yale ambayo ni ya kujiboresha tu na kujipamba kwa ajili ya hafla ya harusi, Iddi na mengineyo.

Hukumu za kisheria zinazohusiana na mavazi ya wanawake hufikia malengo makubwa. Kwa upande wa wanawake, hayo huwapa sifa mahususi, kuwalinda kutokana na macho ya wanaume - mara nyingi - kutokana na kwa vitendo na maneno ya watu waovu. Vile vile mavazi ya kisheria huwapa wanawake uhakikisho, utulivu, heshima na unyenyekevu. Zaidi ya yote, kwa kushikamana na mavazi ya kisheria, mwanamke huwa ametangaza uja wake na unyenyekevu wake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kufuata amri zake na kuepuka makatazo yake, kwa hivyo akawa amestahili kwa hilo baraka zake, kipawa chake, na rehema zake Yeye aliyetakasika.

Ama katika ngazi ya jamii, mavazi ya kisheria ya mwanamke au hijabu yake huilinda jamii nzima kutokana na majaribio, na kuhifadhi utulivu na amani kwa wanajamii wake wote. Kwa maana, majaribio yanapotokea, huharibu jamii pamoja na sehemu zake zote, wanaume na wanawake, na kwa kuanzia hapo, mfumo wa familia, utulivu wake, na uhakikisho wake vinatikiswa na hata vinaweza kupotelea mbali, na hili ni jambo ambalo linaonekana katika nchi nyingi.

Masharti ya hijabu ya mwanamke wa Kiislamu

١
Anapaswa kufunika mwili wote kulingana na maneno ya baadhi ya wanazuoni, au kuufunika isipokuwa uso na viganja viwili kulingana na kauli ya wengineo.
٢
Yenyewe isiwe pambo.
٣
Iwe nzito ambayo haionyeshi kilicho ndani yake.
٤
Iwe pana, sio finyu ili isielezee chochote katika mwili wake.
٥
Isiwe imefukiwa moshi wa manukato wala marashi.
٦
Isiwe inafanana na mavazi ya mwanamume.
٧
Isifanane na mavazi ya makafiri.
٨
Lisiwe vazi la umaarufu.

1. Kuufunika mwili

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." [Al-Ahzab: 59] Wanachuoni walitofautiana kuhusiana na kufunika uso na viganja. Baadhi yao wakasema: ni wajibu, na baadhi yao wakasema: inapendekezwa kufanya hivyo, lakini walikubaliana juu ya ulazima wa kufunika sehemu nyinginezo.

2. Yenyewe isiwe pambo

Hili linaingia katika ujumla wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala wasionyeshe mapambo yao." [Al-Nur: 31]

3, 4. Iwe nzito na pana

Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - amesema: "Aina mbili za watu wa motoni sijawaona bado: watu wenye mijeledi kama vile mikia ya ng'ombe wanawapiga watu kwayo, na wanawake waliovalia, walio uchi, wakengeushao, waliokengeuka wenyewe. Hawataingia Peponi, wala hawatapata harufu yake. Na hakika harufu yake inapatikana kutokea umbali wa hivi na vile." (Muslim 2128) Na imesimuliwa kutoka kwa Usama bin Zaid, Mwenyezi Mungu amrishie kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - alinivisha nguo nzito ya Kikopti, ambayo ilikuwa katika ambavyo Dahiya al-Kalbi alimpa kama zawadi, nami nikamvisha mke wangu. Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie akaniambia, "Kwa nini hukuvaa nguo ile ya Kikopti?" Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nimempa mke wangu kuivaa. Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akaniambia, "Mwamrishe avalie shuka chini yake, kwa maana ninahofia kwamba itaelezea ukubwa wa mifupa yake." (Ahmad 21786)

5. Isiwe imefukiwa moshi wa manukato wala marashi

Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alisema, “Mwanamke yeyote anayetia manukato, kisha akapita karibu na watu ili wapate katika harufu yake, basi yeye amekwisha zini.” (Al-Nasa' i: 5126)

6. Isiwe inafanana na mavazi ya wanamume

Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Abbas - Mwenyezi Mungu amridhie - kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - aliwalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume." (Al-Bukhari 5885)

7. Isifanane na mavazi ya makafiri

Imethibiti katika Sheria kwamba hairuhusiwi kwa Waislamu - wanaume na wanawake - kufanana na makafiri katika ibada zao, siku kuu zao au mavazi ambayo ni mahususi kwao. Kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alisema, “Yeyote anayejifananisha na watu fulani, basi yeye ni mmoja wao.” (Abu Daawuud 4031)

8. Lisiwe vazi la umaarufu

Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - “Yeyote atakayevaa vazi la umaarufu katika dunia hii, Mwenyezi Mungu atamvisha vazi la kumdhalilisha Siku ya Kiyama, kisha atatia ndani yake moto wenye mwako mkali.” (Ibn Majah 3607) Na mavazi ya umaarufu ni kila vazi linalokusudiwa kupata umaarufu miongoni mwa watu.

Masharti yaliyotangulia yanahusu mavazi ya wanawake wa Kiislamu wanapotoka nyumbani, au wanapokuwa mbele ya wanaume wasiokuwa maharamu. Lakini siyo wajibu kwake kushika masharti haya mbele ya mahramu zake au wakati wa kukutana na wanawake wengine. Katika hali hii, anaruhusiwa kupaka manukato na kudhihirisha mapambo kwa udhibiti maalumu.

Kujishaua

Ni wanawake kuwaonyesha wasiokuwa maharamu wao mapambo yake, na uzuri wake miongoni mwa mambo anayopaswa kutowaonyesha.

Vazi la mwanamke wa Kiislamu kulingana na aliye karibu yake

١
Mavazi yake mbele ya wasiokuwa maharamu wake.
٢
Mavazi yake mbele ya maharamu zake wa kiume.
٣
Mavazi yake mbele ya wanawake wengine wa Kiislamu.
٤
Mavazi yake mbele ya wanawake wa Watu wa Kitabu.

Mavazi ya mwanamke wa Kiislamu mbele ya wasiokuwa maharamu wake

Ni hijabu ya kisheria ambayo aliamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake, ambayo imeshatangulia kutajwa masharti yake.

Mavazi ya mwanamke wa Kiislamu mbele ya maharamu wake wa kiume

Ni lazima kwake afunike mwili wake wote mbele yao, isipokuwa kile kinachoonekana mara nyingi, kama vile shingo, nywele, na miguu, pamoja na uso na viganja. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyowamiliki mikono yao ya kiume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yanayohusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa." [Surat Nur: 31]

Mavazi ya mwanamke wa Kiislamu mbele ya wanawake wengine wa Kiislamu

Ni lazima kwake - kama ilivyo mbele ya maharimu wake - afunike mwili wake wote isipokuwa kile kinachoonekana mara nyingi, kama vile shingo, nywele, na miguu, pamoja na uso na viganja. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyowamiliki mikono yao ya kiume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yanayohusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa." [Surat Nur: 31] Na kauli yake, "au wanawake wenzao;" yaani waislamu.

Mavazi ya mwanamke wa Kiislamu mbele ya wanawake wa Watu wa Kitabu

Ni lazima kwake - kama ilivyo kwa wanawake wa Kiislamu - afunike mwili wake wote isipokuwa kile kinachoonekana mara nyingi, kama vile shingo, nywele, na miguu, kwa sababu wanawake wa Watu wa Kitabu walikuwa wakiingia kwa mama za waumini, na haikuwahi fikishwa kuwa Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - aliwaamuru kuvalia hijabu mbele yao.

Aina za mavazi na mapambo ya wanawake kulingana na uhalali na uharamu

١
Mavazi na mapambo yanayoruhusiwa.
٢
Mavazi na mapambo yanayopendekezwa.
٣
Mavazi na mapambo yaliyoharamishwa.

Mavazi na mapambo ya wanawake yaliyoruhusiwa

Hali ya asili ya nguo na mapambo ni kwamba yameruhusiwa, na hakuna kinachoondolewa katika hukumu hii isipokuwa kile ambacho Sheria imeharamisha. Kwa hivyo, mwanamke anaruhusiwa kuvaa aina zote za mavazi, kwa rangi zake zote na aina zote za vitambaa, na ajipambe kwa aina zote za mapambo yanayoruhusiwa kama vile vito, manukato na vipodozi, mradi tu havimdhuru, na wala asijifananishe na makafiri katika hayo, na kwamba vifaa hivyo visiwe vimetengenezwa kwa vitu vilivyoharamishwa kama vile mafuta ya nguruwe kwa mfano.

Mavazi na mapambo yanayopendekezwa

Maana ya hili ni yote yaliyokuja huku yamependekezwa katika Sheria, na vile vile kila kitu ambacho mwanamke huvaa na kujipamba kwacho ili kumfurahisha na kutaka kupendwa na mumewe, mradi tu si haramu.

Mavazi na mapambo yaliyoharamishwa

Maana ya hili ni kila kitu ambacho kimeharamishwa na Sheria na ikatahadharisha dhidi yake miongoni mwa mavazi na mapambo, sawa iwe Sheria imekitaja kwa jina kwamba ni haramu au ni kinyume tu na misingi ya Sheria ambayo imeamriwa kuitii, kama vile kuwakiuka Wayahudi na Wakristo, kutowaiga wanaume, na mfano wa hayo.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani