Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Urithi katika Uislamu

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu baadhi ya sifa za mfumo wa urithi katika Uislamu.

  • Kujua sifa maalumu za hukumu za urithi katika Uislamu.
  • Kujua nguzo na masharti ya urithi.
  • Kuwajua warithi waliokubaliwa kurithi miongoni mwa wanaume na wanawake.

Urithi ni mfumo wa kibinadamu wa kiulimwengu, ambao umma mbalimbali zilizotangulia zamani na za kisasa zilikuwa zikiutumia. Hii ni kwa sababu unafaa silika ya kibinadamu ya kupenda kumiliki vitu na kuvitafuta. Mfumo huu hutatua shida ya namna ya kutumia mali za maiti baada ya kifo chake.

Hukumu za urithi katika sheria ya Kiislamu zina sifa maalumu ya kuzieleza hukumu hizi kwa kina, katika mambo yanayohusiana na hali za mrithishaji, warithi, na fungu la kila mmoja wao katika mfumo jumuishi na wa kuvutia. Miongoni mwa faida za kuelezea kwa kina mfumo wa urithi katika Uislamu ni kutatua sababu za migogoro kati ya jamaa za maiti. Hii ni kwa sababu kama warithi watajua kwamba urithi uligawanywa kati yao kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, roho zao zitatulia, na wataridhia kugawanya kwake. Na miongoni mwa faida zake pia ni kuhifadhi haki za warithi wote, na kwamba jambo hilo halikuachiwa liangaliwe na walifanyie jitihada bidii yao tu, kwa hivyo wakawa wanamzuia wamtakaye na kumpa wamtakaye. Hilo likawa ni sababu ya migogoro na mgawanyiko.

Nguzo za urithi

١
Mrithishaji
٢
Mrithi
٣
Mali inayorithiwa

Mrithishaji

Ni yule aliyekufa - au yule aliye katika hukumu ya wafu - ambaye aliacha kile kinachorithiwa.

Mrithi

Ni wote walio hai baada ya kufa kwa maiti - au yule anayeambatanishwa na walio hai - ambaye anastahili kurithi kutoka kwa maiti kwa sababu ni miongoni mwa sababu za kurithi.

Kinachorithiwa

Ni kile anachoacha mrithishaji (maiti), kama vile mali au haki inayoweza kurithiwa.

Masharti ya urithi

١
Kufa kwa mrithishaji au kuwa kwake katika hukumu ya wafu, kama vile mtu aliyepotea ikiwa jaji atahukumu kwamba amekufa, au yule anayekadiriwa, kama vile kijusi (fetasi) ambaye alitoka mimbani kwa sababu ya jerima ambalo linalazimu aliyemtoa kulipa gharama.
٢
Kuthibitika kwa uhai wa mrithi wakati maiti alipokufa, au kumuingiza katika hukumu ya walio hai kwa kukadiria, kama vile kijusi aliyetoka mimbani ilhali ni hai sawasawa, kwa namna inaonyesha uwepo wake wakati wa kifo cha maiti.
٣
Kujua vyema sababu za kurithi, kama vile ukoo, au ndoa, au kumkomboa mtumwa.

Utaratibu wa kugawanya urithi

١
Kumuandaa maiti kwa ajili ya kumzika
٢
Kulipa madeni yake
٣
Kutekeleza wasia wake
٤
Kugawanya mali yake kati ya warithi wake

Sifa maalumu za urithi katika sheria ya Kiislamu

١
Katika sifa hizo ni kwamba hukumu hizo zilitoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mtukufu, Ajuaye zaidi viumbe wake, na chenye kuwatengeneza na kinachowafaa. Mwenyezi Mungu alisema: "Je, asijue yule aliyeumba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari zote?" [Al-Mulk: 14]
٢
Haikumpa mrithi haki ya kugawa mali yake kama anavyotaka, kwa sababu anaweza kushindwa na matamanio yake, au anaweza kuchukuliwa na hisia zisizozuilika, kwa hivyo akawanyima baadhi ya wanaostahiki au akawaboresha baadhi yao juu ya wenzio bila ya sababu.
٣
Kugawanya mali na kutoiacha iwe tu mikononi mwa watu maalumu, na hilo ni kupitia kuwashirikisha idadi kubwa ya watu katika urithi.
٤
Kudumisha umoja wa familia, mshikamano wake na mfungamano wa wanafamilia wake, kwa kugawa urithi kwa wengi wao, na kwa mfumo wenye uadilifu.
٥
Kuzingatia upande wa mahitaji ya warithi katika kutofautisha kati yao katika mafungu yao ya urithi. Ndiyo tunapata fungu la binti ni nusu ya fungu la kaka yake, kwa sababu kaka yake anahitaji mali kwa kuwa yeye ndiye anayejukumishwa kutoa matumizi ya nyumbani kwake, ilhali dada yake anatunzwa (naye au) na wengine.
٦
Kuzingatia kiwango cha ukaribu wa kiukoo katika kutofautisha kati ya baadhi ya warithi kuliko wengine, kwa sababu ya kuwepo mfungamano wa kimanufaa kati ya mrithi na maiti, ndiyo akatangulizwa baba mbele ya babu, na mama mbele ya nyanya.
٧
Katika mfumo wa Kiislamu, urithi ni wa lazima; kwa hivyo, maiti hawezi kumzuia yeyote kati ya warithi wake kurithi.

Warithi miongoni mwa wanaume

Warithi miongoni mwa wanaume ni kumi. Nao kwa njia ya ujumla ni: Mwana wa kiume, mwana wa mwana wa kiume na wote walio chini yake hata wakishuka chini vipi, baba, babu na wote walio juu yake hata wakipanda juu vipi, kaka, mwana wa kiume wa kaka, ami, mwana wa kiume wa ami, mume na bwana aliyemkomboa maiti huyo utumwani.

Warithi miongoni mwa wanawake

Warithi miongoni mwa wanawake ni aina saba. Nao kwa kifupi ni: binti, binti wa mwana wa kiume na wote wa chini yake hata wakienda chini vipi, mama, nyanya na wote wa juu yake hata wakienda juu vipi, dada, mke, na mwanamke aliyemkomboa maiti huyo kutoka utumwani.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani