Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Wasia na Urithi

Sheria ya Kiislamu inamruhusu Muislamu kufanya wasia wa kutekelezwa baada ya kifo chake. Katika sheria ya Kiislamu kuna mgawanyo mzuri zaidi wa urithi wa maiti. Katika somo hili, utajifunza kuhusu baadhi ya hukumu za wasia na urithi.

  • Kujua makusudio ya wasia.
  • Kujua aina za wasia na hukumu zake.
  • Kujua maana ya urithi.

Maana ya wasia

Wasia ni kumtaka aliyeusiwa kufanya jambo baada ya kifo cha mwenye kuusia, kama vile mwenye kuusia kwamba baadhi ya mali zake zitumike katika kujenga msikiti.

Wasia

Mwislamu ameruhusiwa na sheria kufanya wasia kabla ya kifo chake katika mambo yanayohusiana na mali yake. Amesema Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Haikubaliki kwa Muislamu yeyote ambaye ana kitu chochote cha kuusia, kulala usiku mbili bila ya kuuandika wasia wake na kuwekwa tayari pamoja naye." Ibn Umar akasema: “Haukuwahi kunipita usiku mmoja tangu nilipomsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akisema hivyo isipokuwa nilikuwa tayari nimeshaandika wasia wangu. "(Al-Bukhari 2738, Muslim 1627)

Mwenyezi Mungu Mtukufu alitanguliza utekelezaji wa wasia na kulipa madeni Katika kitabu chake kabla ya kugawanya urithi. Alisema kuhusu urithi, "Baada ya wasia mliousia au kulipa deni." (An-Nisaa: 11)

Hali za wasia

Wasia zina hali kadhaa:

1. Wasia wa wajibu

Ikiwa Mwislamu ana madeni au haki za kimali lakini hakuna ushahidi wowote au nyaraka zinazoonyesha hayo, basi ni wajibu kwake kufanya wasia ili kuzihifadhi haki hizo; kwa sababu kulipa deni ni wajibu, na kile ambacho wajibu hautimii isipokuwa kwa hicho, basi hicho pia ni wajibu.

2. Wasia unaopendekezwa

Ni Mwislamu kuusia sehemu katika mali yake kwamba baada ya kifo chake kipeanwe katika njia za heri, kama vile kuwasaidia baadhi ya jamaa zake masikini na mfano wa hayo. Hilo lina masharti kadhaa:

a) Kwamba wasia huo asiandikiwe yeyote miongoni mwa warithi wake. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alikwisha wagawia mgao wao. Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema, "Mrithi haandikiwi wasia." (Abu Dawood 3565, Tirmidhi 2120, Ibn Majah 2713)

b) Wasia unapaswa kuwa chini ya theluthi moja ya mali, na inaruhusika kuwa theluthi moja ya mali hiyo, lakini ni haramu kufanya wasia kwa zaidi ya theluthi moja. Mmoja wa maswahaba watukufu alipotaka kutoa wasia kwa zaidi ya theluthi moja ya mali zake, Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema; “Theluthi moja, na hata hiyo theluthi moja ni nyingi.” (Al-Bukhari 2744, Muslim 1628)

c) Kwamba mtoa wasia awe ni tajiri, na kwamba mali nyingine ya kutosha iwabakie warithi wake. Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimwambia Sa'ad bin Abi Waqqas, Mwenyezi Mungu amridhie, alipotaka kutoa wasia: "Hakika ikiwa wewe utawaacha warithi wako wakiwa matajiri, ni bora kwako kuliko kuwaacha wakiwa maskini wakiwaombaomba watu." (Al-Bukhari 1295, Muslim 1628)

3. Wasia unaochukiza:

Hii ni ikiwa mali ya mwenye kutoa wasia ni kidogo, na warithi wake wana uhitaji, kwa sababu amewafinya warithi wake. Ndiyo maana Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akamwambia Sa'ad, Mwenyezi Mungu amridhie: “Hakika ikiwa wewe utawaacha warithi wako wakiwa matajiri, ni bora kwako kuliko kuwaacha wakiwa maskini wakiwaombaomba watu." (Al-Bukhari 1295, Muslim 1628)

4. Wasia haramu:

Ni kuusia kufanya kile ambacho kimeharamishwa na Sheria. Kama vile kumuusia mmoja wa warithi wake kama vile mwanawe mkubwa, au mke wake kwa mali fulani na kuwaacha warithi wengineo, au kuusia kwamba wajenge kuba juu ya kaburi lake.

Kiasi cha wasia kinachoruhusiwa

Wasia unaruhusiwa kwa theluthi moja, na hauruhusiwi kuzidisha juu yake, na hata ni bora zaidi kuipunguza iwe chini zaidi. Kwa maana, wakati Sa'ad bin Abi Waqqas, Mwenyezi Mungu amridhie, aliposema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ninausia mali zangu zote? Akasema, "Hapana." Nikasema, "Na nusu?" Akasema, "Hapana." Nikasema, "Na thuluthi moja?" Akasema, "Basi thuluthi moja, na hata thuluthi moja hiyo ni nyingi. Hakika wewe ikiwa utawaacha warithi wako wakiwa matajiri ni bora kuliko kuwaacha wakiwa maskini wakiwaombaomba watu vile vilivyo mikononi mwao." (Al-Bukhari 2742)

Na inaruhusika kufanya wasia wa mali yote badala ya thuluthi moja kwa yule ambaye hana mrithi.

Hukumu ya kutekeleza wasia

Utekelezaji wa wasia wa maiti ni lazima. Mtu ambaye ameamrishwa kuutekeleza wasia ikiwa hatautekeleza, basi atapata dhambi maadamu kuna masharti yanayofanya kuutekeleza kuwa jambo sahihi. Hili ni kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na atakayeubadilisha wasia baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua." (Al-Baqarah: 181)

Urithi

Mtu anapokufa, hana tena haki ya kumiliki mali zake ambazo alichuma katika maisha yake. Uislamu ulituwekea sheria ya kugawanya urithi na kumpa kila mwenye haki, haki yake. Hilo linakuwa baada ya kulipa madeni anayodaiwa maiti na kutekeleza wasia wake.

Qur-ani na Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, vimetubainishia njia ya kugawanya urithi, ili kusiwe na ugomvi baina ya warithi. Kwa hivyo, hakimu katika suala la urithi, ni yule ambaye ndiye hakimu wa mahakimu, Mtakatifu. Kwa hivyo, hairuhusiki kwa mtu yeyote kuibadilisha mirathi au kuigeuza kwa kisingizio kwamba hilo ni kinyume na desturi za nchi na watu. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akasema baada ya aya ya mirathi: "Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Yeye atamtia katika Bustani za mbinguni zipitazo mito chini yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufaulu kukubwa." (An-Nisaa: 13)

Na inawapasa wana wa maiti na jamaa zake baada ya kifo cha jamaa yao, kuwarudia wasomi na mahakimu ili kujua kwa kina jinsi ya kugawanya urithi kisheria, na kukaa mbali na migogoro ya kimali.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani