Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Kuitafakari Qur-ani Tukufu na kuitafsiri

Kuitafsiri Qur-ani Tukufu na kuitafakari ni matendo mawili makuu ambayo humleta Muislamu karibu zaidi, na suala la kujua kile ambacho Mwenyezi Mungu anataka katika maneno yake. Jambo ambalo humsaidia kufanyia kazi yale yaliyo ndani yake. Katika somo hili, utajifunza maana ya kutafakari, tafsiri na umuhimu wake.

  • Kujua maana ya tafsiri ya Qur-ani Tukufu na kuitafakari.
  • Kujua hadhi ya kutafakari na kutafsiri, na hitaji lililoko juu ya hayo.
  • Kujua njia za kutafsiri Qur-ani Tukufu.
  • Kujua vitabu muhimu zaidi na vya kuaminika vya tafsiri.

Kutafsiri na kutafakari Qur-ani Tukufu

Kila Muislamu anapaswa kuwa na hima kubwa kuisoma Qur-ani Tukufu kwa usahihi, kutafakari maana zake, amri zake, makatazo yake, kujifunza tafsiri yake na hukumu zake, kisha kuifanyia kazi ili aweze kupata furaha ya dunia hii na Akhera.

Maana ya kutafakari

Kutafakari ni kusimama kwenye aya na kufikiria kwa kina yale yaliyo ndani yake; ili kufaidika na kuitekeleza.

Mwenye kuzitafakari aya za Qur-ani Tukufu anapaswa kujua maana ya jumla ya aya hizo, ili kutafakari kwake na kuzifahamu kwake kuwe sahihi.

Hadhi ya kutafakari Qur-ani Tukufu

Kila Muislamu analazimika kuitafakari Qurani hii kuu, na aelewe aya na maana zake, na kwamba aishi pamoja nayo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake na wawaidhike wenye akili." [Swad: 29] Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, hawaizingatii hii Qur-ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?" [Muhammad: 24]

Maana ya tafsiri

Tafsiri ni kubainisha maana za Qur-ani Tukufu.

Umuhimu wa tafsiri na hitaji lililoko juu yake

Elimu ya ufasiri ni moja ya elimu zenye manufaa na tukufu zaidi. Hii ni kwa sababu inahusiana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na husaidia kuelewa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kujua kile alichokusudia. Na kupitia elimu ya ufasiri zinajulikana maana za Qur-ani Tukufu, ambazo humsaidia Muislamu kuongoka na kufikia kutenda matendo mema na kupata ridhaa ya Mwenyezi Mungu aliyetakasika, aliyetukuka, na kufuzu kuingia katika Pepo zake. Na hayo ni kwa kufanya maamrisho yake yaliyokuja katika Kitabu chake kitukufu, na kujiepusha na makatazo yake, na kuchukua somo kutoka katika visa vyake, na kuzisadiki habari zake.Na kwa kujua tafsiri mwanadamu anapata kutenganisha kati ya haki na batili, na kuondoa mkanganyiko wowote unaoweza kuzuia kufikia maana za aya na vitu ambavyo zinaashiria kiuhakika.

Juhudi ya Maswahaba katika kujua maana za Qur-ani na tafsiri yake kutoka kwa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Maswahaba watukufu, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, walikuwa wakimuuliza Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuhusu yale yanayowatatiza kuyaelewa katika Qur-ani. Imesimuliwa kutoka kwa 'Abdullah bin Mas'ud, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kuwa alisema ilipoteremka Aya hii, "Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhuluma." [Al-An'am: 82] Jambo hili likawawia gumu maswahaba wa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na wakasema: "Ni nani miongoni mwetu ambaye hajaidhulumu nafsi yake?" Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema: "Si kama mnavyofikiri. Bali ni kama Luqman alivyomwambia mwanawe: 'Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhuluma iliyo kubwa.'" [Luqman: 13] (Al-Bukhari 6937, na Muslim 124)

Katika kutafsiri Qur-ani Tukufu na kujua maana zake, njia zifuatazo zinatumika:

١
Kutafsiri Qur-ani kwa Qur-ani.
٢
Kutafsiri Qur-ani kwa Sunna.
٣
Tafsiri ya maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao.
٤
Tafsiri ya wale waliokuja baada ya maswahaba.

Kwanza: Kutafsiri Qur-ani kwa Qur-ani

Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyeiteremsha, naye ndiye ajuaye zaidi yale aliyoyataka.

Kama vile kauli yake Mtukufu: "Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na hofu wala hawatahuzunika. Wale ambao waliamini na wakawa wanamcha Mungu." (Yunus:62-63) Hapa alitafsiri maana ya "vipenzi vya Mwenyezi Mungu" kwa kauli yake, "Hao ni ambao waliamini na wakawa wanamcha Mungu."

Pili: Kutafsiri Qur-ani kwa Sunna

Kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ndiye anayefikisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo yeye ndiye ajuaye zaidi ya watu wote kile ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu alikusudia katika maneno yake.

Imesimuliwa kutoka kwa Uqba bin Amir kuwa: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akisema hali ya kuwa yuko juu ya mimbari: "Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo" [Al-Anfal: 60] Sikilizeni! Hakika, nguvu ni kutupa mishale. Sikilizeni! Hakika, nguvu ni kutupa mishale. Sikilizeni! Hakika, nguvu ni kutupa mishale." (Muslim 1917)

Pili: Tafsiri ya maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao

Wao ndio wajuao vyema hili; kwa sababu walishuhudia matukio na hali mbalimbali ambazo wao tu ndio walioziona, na tena kwa sababu ya ufahamu wao kamili, elimu yao sahihi na matendo yao mema.

Miongoni mwa mifano ya hilo ni pamoja na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na mkiwa wagonjwa, au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake." [An-Nisaa: 43] Hapa imethibiti kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kwamba alitafsiri "mmewagusa wanawake" kwamba ni tendo la ndoa (Tafsir Twabari 8/389)

Nne: Tafsiri ya wale waliokuja baada ya maswahaba

Nao ni wale waliokuwa na hamu kubwa ya kuchukua tafsiri kutoka kwa Maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kwa sababu hao ndio watu bora baada ya Maswahaba, na wao ndio waliosalimika zaidi kutokana na matamanio kuliko wale waliokuja baada yao.

Wajibu wa Muislamu katika kutafsiri Qur-ani

Muislamu anapopatwa na kitu kinachomsumbua katika kuelewa Qur-ani na kujua maana zake, basi anapaswa kurejelea vitabu vya tafsiri na maneno ya wanazuoni ambao wamebobea katika tafsiri na ambao ni wa kutegemewa katika hilo.

Kutafsiri Qur-ani Tukufu si jambo ambalo kila Muislamu anaweza kulifanya, bali ni jambo ambalo wanafaa kulifanya watu wenye elimu hii ya kutafsiri. Kwa hivyo Waislamu wa kawaida hawafai kufanya hivyo bila ya kuwa na elimu hii. Kwani, mfasiri ni mkalimani wa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na anamshuhudia yale aliyokusudia, na ni lazima autukuze ushahidi huu, ahofu kusema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu akaja kuingia katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliharamisha, akaja kuhizika kwa sababu ya hilo Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Sema: Mola Mlezi wangu ameharamisha mambo machafu ya dhahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asichokiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua." [Al-Araf: 33]

Vitabu muhimu zaidi vya kuaminika katika tafsiri

Kuna vitabu vingi vilivyoandikwa katika tafsiri ya Qur-ani Tukufu. Na kwa vile haviko katika kiwango sawa katika suala la kukubalika kwake, ni wajibu kwa Muislamu kutegemea tafsiri za kuaminika, ambazo waandishi wake walizingatia kanuni za ufasiri. Miongoni mwa vitabu hivi maarufu ni:

Vitabu muhimu zaidi vya tafsiri

١
Tafsir Jami' al-Bayan an Ta-wil Aay al-Qur-an, cha Ibn Jarir, At-Twabari.
٢
Tafsiri Al-Qur-an Al-Adhwim, cha Imam Ibn Kathir Ad-Dimashqi.
٣
Taysir Al-Karim Ar-Rahman fi Tafsir Kalaam Al-Mannan, cha Sheikh Abdur-Rahman As-Sa'adi.
٤
At-Tafsir Al-Muyassar, kilichoandikwa na kundi la wasomi, kilichochapishwa na Kiwanda cha Kuchapisha Qur-ani Tukufu cha mfalme Fahad huko Madina.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani