Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Ujumbe wa Nabii Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwatuma Mitume kwa ajili ya hekima kubwa, na akafanya wa mwisho wao kuwa Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akamboresha kuliko wengine wote. Katika somo hili, utajifunza kuhusu baadhi ya hekima hizi, na kuhusu haki za Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, juu ya umma wake.

  • Kujua hekima ya kutumwa Mitume, amani iwe juu yao.
  • Kuhisi ubora wa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, juu ya wengineo wote.
  • Kujua baadhi ya haki za Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, juu ya umma wake.

Hitaji la wanadamu juu ya Mitume

Hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ilihitaji kwamba atume mwonyaji katika kila umma, ili awabainishie yale ambayo Mwenyezi Mungu amewateremshia waja wake ya Dini na uwongofu, ambayo kwayo watatengenea katika dunia yao na akhera yao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na hapana umma wowote ila ulipata mwonyaji kati yao." [Fatir: 24]

Kwa maana hakuna njia ya furaha na mafanikio, siyo katika ulimwengu huu, wala katika Akhera, isipokuwa mikononi mwa Mitume. Na hakuna njia ya kujua mema na mabaya kwa undani isipokuwa kutoka kwao. Na wala radhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu haipatikani isipokuwa mikononi mwao. Kwa maana, matendo mazuri, kauli nzuri na maadili bora si isipokuwa mwongozo wao tu na yale waliyokuja nayo.

Kumuamini Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwamba ni Mtume

Tunaamini kuwa Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kwamba yeye ndiye bwana wa watu wa kale na wale wa mwisho, na kwamba yeye ndiye mwisho wa Manabii. Kwa hivyo, hakuna Nabii yeyote baada yake. Alikwishafikisha ujumbe, akatekeleza amana, na akashauri umma wake, na akapambana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu haki ya kupambana kwa ajili yake.

Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu." (Al-Fat-h: 29)

Ni lazima juu yetu tumsadiki katika yale aliyotuambia, tumtii katika yale aliyoamrisha, tujiepushe na yale aliyokataza na kukemea, na kwamba tumwabudu Mwenyezi Mungu kulingana na Sunna yake, na kwamba tufuate mfano wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Mwisho wa Mitume na Manabii

Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ndiye mwisho wa Mitume na Manabii, na hakuna Nabii yeyote baada yake. Ujumbe wake ndio hitimisho la ujumbe wa kimungu, na dini yake ndiyo ya mwisho kabisa.

Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii." (Al-Ahzab: 40)

Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kutoka kwa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa alisema: "Hakika, mfano wangu na mfano wa Manabii wa kabla yangu ni mfano wa mtu aliyejenga nyumba na akaiboresha na akaifanya kuwa nzuri, isipokuwa mahali pa tofali moja katika pembe moja. Kwa hivyo watu wakawa wanaizunguka na kuifurahia na kusema, 'Kwa nini halikuwekwa tofali hili?'" Akasema, "Mimi ndiye tofali hilo, na mimi ndiye mwisho wa Manabii." (Al-Bukhari 3535)

Mtume na Nabii bora zaidi

Nabii wetu Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ndiye bora kabisa katika Manabii, na ndiye bora kabisa katika viumbe vyote, na mwenye cheo kikubwa zaidi yao wote kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mwenyezi Mungu Mtukufu aliinua cheo chake akawa ndiye wa kuheshimika zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtakatifu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hekima na amekufundisha yale uliyokuwa huyajui. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zilizo juu yako ni kubwa." [Nisaa: 113] Na Mwenye nguvu, Mtukufu zaidi akasema akimwambia Nabii wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Na tukakunyanyulia utajo wako." [Ash-Sharh: 4]

Yeye ndiye bwana wa wanadamu wote, na wa kwanza ambaye kaburi lake litafunguka, na mwombezi wa kwanza atakayekubaliwa uombezi wake, na mkononi mwake kutakuwa bendera ya kumsifu Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, na wa kwanza kuvuka Njia iliyo juu ya Moto wa Jahannam, na wa kwanza kubisha mlango wa Bustani za mbinguni, na wa kwanza kuingia ndani yake.

Rehema kwa walimwengu

Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad kuwa ni rehema kwa walimwengu wote, hivyo basi ujumbe wake ni wa jumla kwa vizito viwili: wanadamu na majini, na ujumbe wake ni wa jumla kwa watu wote. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Nasi hatukukutuma ila uwe ni rehema kwa walimwengu wote." (Al-Anbiya:107)

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Na hatukukutuma ila kwa watu wote." (Sabaa: 28) Na alisema, “Sema: Enyi watu, hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote.” (Al-A'raf: 158)

Mwenyezi Mungu alimtuma kama rehema kwa ulimwengu ili kuwatoa katika giza la ushirikina, ukafiri na ujinga, hadi kwenye nuru ya elimu, imani na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, ili wapate kwa hayo msamaha wa Mwenyezi Mungu, radhi zake, na waepuke kutokana na adhabu yake na ghadhabu yake.

Ulazima wa kumwamini na kuufuata ujumbe wake

Ujumbe wa Muhammad unafutilia mbali jumbe zilizopita zamani. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu hatakubali dini yoyote kutoka kwa mtu yeyote isipokuwa tu kumfuata Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Hakuna mtu yeyote anayeweza kufikia neema ya Bustani za mbinguni isipokuwa kwa kupitia njia yake, kwa kuwa yeye rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ndiye mtukufu zaidi miongoni mwa Mitume, na umma wake ndio umma bora, na sheria yake ndiyo sheria kamilifu zaidi miongoni mwa sheria zote.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, "Na anayetafuta dini isiyokuwa Uislamu, haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kuhasiri." (Al-Imran: 85)

Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira, kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa alisema: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko katika mkono wake, hatasikia yeyote kunihusu katika umma huu, awe ni Myahudi au Mkristo, kisha akafa na wala asiamini yale niliyotumwa nayo, isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni.” (Muslim 153)

Miongoni mwa miujiza ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, inayoonyesha kwamba yeye ni Mtume

Mwenyezi Mungu Mtukufu alimuunga mkono Mtume wetu Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa miujiza ya ajabu, na ishara zenye kufumbua macho, ambazo ndani yake kuna ishara na ushahidi juu ya ukweli wa unabii wake na ujumbe wake. Miongoni mwa miujiza hiyo ni:

Qur-ani Tukufu

Ishara kubwa zaidi aliyopewa Mtume wetu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ni Qur-ani Tukufu, ambayo inazungumzisha roho na akili. Na ni ishara ya kudumu hadi Siku ya Hukumu, ambayo haifikiwi na mabadiliko yoyote au mageuzi, kwani ni muujiza katika lugha yake na mtindo wake, na ni muujiza katika sheria zake na hukumu zake, na ni muujiza katika habari zake.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Sema: Wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa Qur-ani hii, basi hawangeweza kuleta mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao." (Al-Israa: 88)

Kupasuka mwezi

Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Saa imekaribia, na mwezi umepasuka! Na wakiona Ishara, hugeuka upande na husema: Huu ni uchawi tu unazidi kuendelea." [Al-Qamar: 1, 2] Kisa hiki cha kupasuka mwezi kilitokea katika maisha ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na Maquraishi na wengineo wakauona.

Kuongezeka kwa chakula kidogo mikononi mwake

Hili lilipotokea, watu waliokuwa pamoja naye walikula kwacho na tena kikabaki. Hilo lilikuja kutoka kwa Samura bin Jundab, kuwa alisema: "Tulikuwa pamoja na Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akaletewa bakuli lenye mchuzi ndani yake." Akasema: "Basi akala, na watu hao pia wakala. Kisha watu hao wakaendelea kubadilishana bakuli hilo mpaka karibia wakati wa adhuhuri. Walikuwa wanakula kisha wananyanyuka. Kisha watu wengine wanakuja na kukichukua." (Musnad Ahmad 20135)

Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kujulisha juu ya mambo ya ghaibu

Katika ishara zake ni kwamba alikuwa akijuliaha mambo ya ghaibu, kisha yanatokea kama alivyojulisha. Na tayari yamekwisha fanyika mengi katika yale aliyojulisha juu yake, na hata bado tunaendelea kuona mambo mbalimbali katika yale aliyojulisha.

Imesimuliwa kutoka kwa Anas, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa alisema 'Umar ibn al-Khattab Mwenyezi Mungu amridhie, alianza kuongea juu ya watu wa Badr. Alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa akituonyesha mahali pa kuuawa kwa watu wa Badr jana, akisema, “Hapa ni mahali pa kufia pa fulani kesho, Mwenyezi Mungu akipenda." Umar akasema, "Ninaapa kwa Yule ambaye alimtuma kwa haki, watu hao hawakuruka mipaka aliyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu." [Muslim 2873]

Haki za Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, juu ya umma wake

Haki za Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, juu ya umma wake ni nyingi, ikiwa ni pamoja na zifuatazo:

1. Kuamini unabii wake

Kuamini unabii wake na ujumbe wake, na kuamini kwamba ujumbe wake ulifutilia mbali jumbe zote zilizotangulia.

2. Kumsadiki

Kumsadiki katika yale aliyosema, na kumtii katika yale aliyoamuru, na kujiepusha na yale aliyokataza na akayakemea, na kwamba hapaswi kuabudiwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kama alivyoweka katika sheria. Mwenyezi Mungu Mtukufu, alisema: “Na anachowapa Mtume, kichukueni. Na anachowakataza, jiepusheni nacho." (Al-Hashr: 7)

3. Kukubali yale aliyokuja nayo Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Inatulazimu kukubali yale aliyokuja nayo Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, tufuate Sunna yake, tuuheshimu na kuutukuza mwongozo wake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "La! Ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayohitilafiana ndani yake, kisha wasione uzito wowote katika nyoyo zao juu ya hukumu utakayotoa, na wanyenyekee kabisa." [An-Nisaa: 65]

4. Kujitahadharisha kutokana na kukiuka amri zake

Lazima tujihadhari kutokana na kukiuka amri za Nabii, kwa sababu kukiuka amri zake ni sababu ya kuingia katika majaribio, upotovu na adhabu chungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Basi na watahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu." [An-Nur: 63]

5. Kutanguliza upendo wake mbele ya upendo wa mwanadamu yeyote

Tunapaswa kutanguliza upendo wa Nabii mbele ya upendo wa nafsi zetu, baba zetu, watoto wetu, na viumbe wengine wote. Imesimuliwa kutoka kwa Anas (bin Malik) kuwa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Hataamini mmoja wenu mpaka niwe mpendwa zaidi kwake kuliko mzazi wake, mtoto wake, na watu wote." (Al-Bukhari 15) Na Umar bin Khattab, Mwenyezi Mungu amridhie, alisema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, wewe ni mpendwa zaidi kwangu kuliko kila kitu isipokuwa mimi mwenyewe." Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema: "Hapana, ninaapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, mpaka niwe mpendwa zaidi kwako hata kujiliko wewe mwenyewe." Umar akamwambia: "Sasa, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wewe ni mpendwa zaidi kwangu hata kujiliko mimi mwenyewe." Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema: "Sasa, ewe Umar." (Al-Bukhari 6632)

6. Kuamini kwamba alifikisha ujumbe

Ni lazima kuamini kwamba Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alifikisha ujumbe wote, akatimiza amana yake, na akaushauri umma. Hakuna heri yoyote isipokuwa aliyouonyesha umma wake na akawahimiza kuifanya, wala hakuna uovu wowote isipokuwa aliukataza umma wake na akawatahadharisha nao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini." [Al-Ma’idah: 3]

Masahaba wa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, walishuhudia kwamba Nabii alifikisha ujumbe katika mkusanyiko wao mkubwa zaidi siku aliyowahutubia wakati wa Hija ya kuaga. Katika hadithi ya Jabir, Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Na nyinyi mtaulizwa kunihusu, basi mtasemaje?" Wakasema: "Tunashuhudia kwamba ulifikisha, ukatekeleza na ukanasihi." Kwa hivyo, akaonyesha kwa kidole chake cha shahada, akikiinua juu mbinguni kisha anakielekeza kwa watu: "Ewe Mwenyezi Mungu shuhudia. Ewe Mwenyezi Mungu shuhudia." mara tatu (Muslim 1218)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani