Sehemu ya sasa:
Somo Janga la ugonjwa ni somo na mawaidha
:idadi wanafunzi wengine walimaliza somo hili
Janga la magonjwa ni moja ya majaliwa ya Mwenyezi Mungu yanayoteremka juu ya watu, Waislamu wao na makafiri wao. Lakini hali ya Muislamu anapokuwa katika balaa (janga) si sawa na ile ya wengineo; kwani yeye huamiliana nayo kwa yale ambayo Mola wake Mlezi Mtukufu aliamuru,kama vile kuwa na subira na kufanya sababu za kisheria za kuizuia kabla ya kutokea kwake, na kutafuta tiba baada ya kushikiwa nayo.
Katika kuenea kwa majanga ya magonjwa kwa sababu ya kiumbe dhaifu ambacho hakiwezi kuonekana isipokuwa kwa kutumia darubini, na yakasababisha hofu na kufadhaika kukubwa katika roho za watu - kama ilivyokuwa katika janga la Corona - kuna ishara inayoonyesha nguvu kubwa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na udhaifu wa viumbe. Hata kama watafikia vipi katika maendeleo na wakamiliki teknolojia ya namna gani, hawawezi kutoka nje ya duara la udhaifu wa kibinadamu. Na pia kuna ishara kwamba Mwenyezi Mungu ana nguvu kubwa madhubuti, ambayo hakuna kitu duniani wala mbinguni kinachoweza kumshinda.
Mipangilio ya Mwenyezi Mungu na kadari yake ni haki
Kwa hivyo, Waislamu wanaamini kwamba kila kitu ulimwenguni kilipangwa na Mwenyezi Mungu na akakiandika kabla ya kuumba viumbe. Itikadi hii inawafanya kuwa na utulivu na udhabiti wakati wa hofu. Kwa hivyo wanaipokea mipangilio ya Mwenyezi Mungu kwa vifua vilivyokunjuka.
Kupata mawaidha na kuzingatia:
Misiba na balaa inayompata Mwislamu ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:
Miongoni mwa matendo makuu ya ibada wakati wa misiba hii ni kuwa mja anayemuomba Mwenyezi Mungu dua kwa unyenyekevu, uvunjifu, na kumtii. Pia ni kuwa mja mwenye kuomba kuokolewa na kuondolewa balaa hiyo na Mwenyezi Mungu peke yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwa nini wasinyenyekee ilipowafika adhabu yetu? Lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu, na Shetani akawapambia yale waliyokuwa wakiyafanya." (Al-An 'am 43) Dua ya dhati inamfungulia mtu milango ya mbinguni, na inapenya ndani ya pazia, na inakunja umbali mrefu, na kumleta mja karibu na Mwingi wa rehema. "Na waja wangu watakapokuuliza habari zangu, waambie kuwa Mimi hakika nipo karibu. Ninaitikia maombi ya mwombaji anaponiomba." [Al-Baqara: 186] Wahab bin Munabbih, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema: 'Balaa hushuka ili itoe nje dua.'
Mojawapo ya kudanganyika kukubwa zaidi na kufikiri kwamba tuko salama dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu ni kuamini kwamba tuna kinga dhidi ya misiba hii na milipuko ya magonjwa. Na kwamba jambo la mwisho tunalofikiria ni uwepo wa uhusiano kati ya balaa hizo na dhambi zetu, pamoja na kwamba haya ni katika misingi ya Qur-ani ambayo yamethibiti katika aya zaidi ya moja. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Nyinyi, ulipokusibuni msiba ambao nyinyi mmekwisha watia mara mbili mfano wa huo, mnasema: 'Umetoka wapi huu?' Sema: "Huo umetoka kwenu wenyewe." (Al-Imran 165) na alisema: "Na misiba inayokusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi." (Ash-Shura: 30)
"Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake."
Kuwa na imani na Mwenyezi Mungu na kumtegemea ni mojawapo ya njia kuu za kushinda majaribio na balaa. Kwa hivyo mtu anapaswa kuwa na yakini kwamba faraja iko karibu. Pia eneza matumaini katika wale walio karibu nawe na uepukane na kuwa na wasiwasi na kutokuwa na matumaini; kwa maana ugumu mmoja hauwezi kushinda wepesi mbili: "Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi. Hakika pamoja na uzito upo wepesi." (Ash-Sharh: 5, 6)
Miongoni mwa desturi za Mwenyezi Mungu alizoweka ulimwenguni ni kwamba; kufanya sababu za kisheria zinazowezekana, kuwa ni mojawapo ya sababu za kuzuia maovu. Na hivyo ndivyo walivyofanya Mitume na watu wema. Na hilo ni katika kumtegemea Mwenyezi Mungu kikamilifu, na kufikia kuwa mja wake sawasawa.
Kiumbe kilichofichikana ambacho kimewanyima watu wa duaniani furaha yao, raha zao, usalama wao, utulivu wao na maisha yao ya kawaida. Basi, je, nafaa kwa mtu mwenye akili timamu, achilia mbali Muumini, kuichukua dunia hii kama mahali pa kutua, pa kuipigania na pa kushindana juu ya mambo yake yasiyo na thamani?
Hakuna shaka kwamba virusi hivi ni miongoni mwa ishara za Mwenyezi Mungu za kimaumbile ya kiulimwengu, ambazo kwazo Mwenyezi Mungu huwahofisha waja wake, na anawasukuma kwazo ili kuwapa mawaidha na waweze kuzingatia, na kufufua uja wa kumhofu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Nasi hatutumi Ishara ila kwa ajili ya kuhofisha." (Al-Israa: 59)
Kuhuisha uja wa mtu kuwa na hofu ni katika ishara za Mwenyezi Mungu:
Muda ndio mtaji mkuu wa Muislamu katika dunia hii, nao ndio mali yenye thamani kubwa zaidi kuliko thamani nyingine ile. Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu amridhie, alisimulia kutoka kwa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwamba alisema: "Kuna neema mbili ambazo watu wengi hupunjika ndani yake; Afya njema na wakati wa mapumziko." (Al-Bukhari 6412)