Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Hukumu zinazohusiana na magonjwa ya milipuko

Somo hili linabainisha masuala mbalimbali ya kisheria na masuala yanayohusiana na magonjwa ya milipuko na maradhi ya kawaida.

  • Kujifunza kuhusu baadhi ya hukumu na ushauri muhimu kuhusiana na magonjwa ya milipuko na maradhi ya kawaida.

1. Kutumia dawa na chanjo:

Inaruhusiwa kufanya chanjo kwa ajili ya kuzuia kabla ya kutokea kwa ugonjwa, na siyo kinyume na kumtegemea Mwenyezi Mungu.Kwani Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema katika hadithi sahihi: "Mwenye kula 'Ajwa saba kila asubuhi kila siku, basi hatadhurika na sumu wala uchawi katika siku hiyo." (Al-Bukhari 5445, Muslim 2047) Na hili ni kuzuia balaa kabla haijatokea.

2. Kuwatenga wenye maradhi yanayofanana:

Sheria ilihimiza kuepukana na suala la kuchanganyika kwa wagonjwa na watu wenye afya njema. Amesema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Mgonjwa asiende aliko mwenye afya nzuri." (Bukhari 5771, Muslim 2221)

Kwa hivyo, anafaa asiingie aliko mgonjwa wa ugonjwa wa kuambukiza. Lakini anaweza kuwatembelea familia yake na kuwauliza juu ya hali yake, kumwombea dua na kusaidia kupata dawa kwa njia iwezekanayo kama vile kutoa mali, na kuipata kupitia heshima yake na mengineyo; huku ukichukua sababu za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

3. Kuzuia kusafiri kwenda au kutoka katika eneo lenye janga:

Hairuhusiwi kuingia au kutoka katika eneo ambalo kuna tauni. Na hili ni kwa mujibu wa hadithi ya Abdur-Rahman bin 'Auf, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Mnaposikia juu yake (yaani, kuenea kwa tauni) katika nchi fulani, basi msiende huko, na kama itatokea (yaani, tauni) katika nchi ambapo mpo, basi msiondoke katika nchi hiyo mkiikimbia (hiyo tauni)." (Bukhari 5729, Muslim 2219) Hivi ndivyo wanavyoona wengi wa wanazuoni, kwamba hairuhusiwi kusafiri kwenda nchi ambayo janga kama hilo limetokea au kutoka ndani yake ili kuepuka ugonjwa huo.

4. Kuacha swala ya jamaa (mkusanyiko):

Swala ya mkusanyiko ni ya lazima kwa wanaume. Lakini wanazuoni walisema kuwa haiwi lazima kunapokuwa na udhuru kwa kinachokubaliwa kisheria. Na pia kulingana na hadithi ya 'Aisha, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alipougua, hakuwa akiwaswalisha watu. Na akasema: "Mwamrisheni Abu Bakr awaswalishe watu." (Bukhari 664, Muslim 418) Basi hilo likaonyesha kwamba ikiwa Mwislamu ana udhuru wa ugonjwa au ugumu wa dhahiri, anaruhusiwa kuacha kuswalia katika jamaa ya msikitini na anaweza kuswali peke yake.

5. Kuweka msikiti nyumbani:

Inapendekezwa kwa Muislamu kutengeneza ndani ya nyumba yake msikiti kwa ajili ya kuswalia humo swala za wajibu ikiwa zinapita kwa sababu ya udhuru. Na pia aswalie humo swala za hiari, na huo ndio mwongozo wa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Katika hadithi ya 'Itaban bin Malik, Mwenyezi Mungu amridhie, ambayo ilisimuliwa na Muslim, ni kwamba alimwambia Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwamba mw macho yake yalikuwa yamedhoofika, na kwamba mafuriko yanapotokea, kunakuwa na bonde la mafuriko linalozuia kati yake na watu wake ambalo haweza kwenda hivyo msikitini kwao. Kwa hivyo akamuomba Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwamba amtembelee nyumbani kwake na aswalie ndani yake; ili apafanye mahali atakaposwalia Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mahali pake pa kuswalia. Basi Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akaja na akaswalia ndani yake rakaa mbili.

Vivyo hivyo, Maimuna, Mwenyezi Mungu amridhie, alikuwa na msikiti nyumbani kwake. Na 'Ammar bin Yasir pia. Kwa hivyo, tunapaswa kuchukua fursa ya hali hizi mpya na kwamba tuwe na misikiti katika nyumba zetu.

6. Ruhusa ya kuswalia swala ya jamaa nyumbani:

Inaruhusiwa kuswalia swala ya jamaa nyumbani wakati ambapo haiwezekani kuiswalia msikitini. Na walioswali hivyo wanapata malipo ya swala ya jamaa. Imethibiti ruhusa ya kuswalia swala ya jamaa nyumbani kutoka kwa kundi la maswahaba kama vile Ibn Masud na Anas, Mwenyezi Mungu awaridhie, na wengineo wakati mtu anakosa kuswali pamoja na Imamu.

7. Ni nani anafaa zaidi kuwa Imamu?

Lakini ikiwa hatakubali kuswalisha, basi anayefaa zaidi kuwa imamu atakuwa ni yule anayesoma vyema zaidi Kitabu cha Mwenyezi Mungu.Lakini ikiwa watakuwa sawa, basi atakayefaa zaidi ni yule ambaye anajua zaidi hukumu za swala.Lakini ikiwa watakuwa sawa, basi mzee zaidi kati yao.

8. Mahali ambapo maamuma anafaa kusimama:

Ikiwa Muislamu ataswalia nyumbani kwake, ikiwa maamuma ni mwanamume, basi Sunna ni kwamba asimame upande wa kulia wa imamu ikiwa ni mmoja, na ikiwa ni zaidi ya mmoja, basi Sunna ni kwamba wasimame nyuma yake. Na ikiwa maamuma ni mwanamke, basi Sunna ni kwamba awe nyuma yake, na ikiwa wanaume na wanawake watakusanyika, basi wanaume watasimama nyuma ya imamu, kisha wanawake watakuwa nyuma yao.

Fursa:

Matukio haya mageni ni fursa kubwa ya kuwafundisha wana familia jinsi ya kuswali, masharti yake, hukumu za usafi na kile kinachohitajika ndani yake. Na kuwausia kuendelea kufanya hivyo.

9. Swala ya wanawake katika jamaa:

Wanawake wanaruhusiwa kuswalia katika jamaa majumbani. Kwa sababu hili linathibitika kutoka kwa Umm Waraqa, 'Aisha, na Umm Salama, Mwenyezi Mungu awe radhi nao. Na hilo ni bora zaidi kwao na lenye malipo makubwa zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Imamu wao atasimama katikati ya safu.

10. Kuhudhuria kwa mtu aliyeambukizwa na maradhi katika swala ya jamaa au mikusanyiko:

Ni marufuku kwa mtu aliyeambukizwa na janga la kuambukiza kuhudhuria mikusanyiko ya watu, kwa sababu ya madhara ambayo hii husababisha kwa watu. Na Mwenyezi Mungu anasema: "Na wale wanaowaudhi Waumini wanaume na wanawake pasi na wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhuluma kubwa na dhambi zilizo dhahiri." (Al-Ahzab: 58)

Miongoni mwa kanuni za kisheria zilizothibiti ni kwamba: Hakuna kuwadhuru watu wala kujidhuru mwenyewe. Kwa hivyo hairuhusiwi kwa wale ambao wameambukizwa ugonjwa kuchanganyika na wale ambao ni wenye afya nzuri. Amesema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Mgonjwa asiende aliko mwenye afya nzuri." (Al-Bukhari 5771, Muslim 2221)

11. Kuvaa barakoa katika swala:

Ni jambo la kuchukiza kwa mtu anayeswali kuufunika mdomo wake. Kwani Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikataza hilo. Lakini kama kuna haja ya kufanya hivyo au ikiwa kuna hofu ya kudhurika kutokana na magonjwa yanayoambukizana, basi mtu anaweza kuvaa barakoa.

12. Hukumu za siku ya Ijumaa:

Iwapo haitawezekana kuswali swala ya jamaa, basi hukumu za siku ya Ijumaa zitabaki. Kwa hivyo inaruhusika kusoma Surat Sajda na Al-Insan katika swala ya Fajr, na kuomba dua katika saa ya kujibiwa dua, ambayo ni masaa ya mwisho baada ya swala ya Asr, na kumswalia sana Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mchana wake, na kusoma Suratul-Kahf. Kwani hali ya asili ni kwamba hukumu hizi zote zinaruhusika, na kwamba hazifuatani na swala.

13. Kuacha kusalimiana mkononi:

Kusalimiana mikono ni sunna. Amesema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakuna Waislamu wawili wanaokutana na kusalimiana mikononi isipokuwa wanasamehewa kabla hawajatengana." (Abu Dawud 5212) Lakini ikiwa Muislamu atahofia maambukizi kwa sababu ya kusalimiana mikononi, basi itamtosha kutoa salamu kwa mdomo tu. Na inatarajiwa kwamba ataandikiwa malipo ya kusalimiana mkononi Mwenyezi Mungu akipenda.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani