Sehemu ya sasa:
Somo Kamari na Maysir
Kamari au maysir ni nini?
Kamari ni kila mchezo ambao upande mmoja au zaidi unapata faida na mwingine unapata hasara. Kwa hivyo kila mshiriki huwa kati ya kupata faida (mali au mengineyo), au kupata hasara ya mali hiyo au mengineyo.
Kamari imeharamishwa kwa Kitabu (Qur-ani), Sunna na maafikiano ya wanazuoni.
Mshindi katika kamari na maysir hupata faida, lakini Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu alibainisha kwamba dhambi zake na madhara yake ni makubwa kuliko faida zake na manufaa yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Wanakuuliza juu ya mvinyo na kamari. Sema: Katika hivyo, zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake." (Al-Baqarah: 219)
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Enyi mlioamini! Bila ya shaka mvinyo, na kamari, na masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika matendo ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mfaulu." (Al- Maaidah: 90)
Madhara ya kamari na maysir kwa mtu binafsi na jamii:
1. Kila mchezo ambao mshindi huchukua kitu kutoka kwa mshindwa: kama vile kikundi cha watu wanaocheza kadi, na kila mmoja wao akaweka kiasi fulani cha mali, kwa hivyo yeyote atakayeshinda, anachukua mali hizo zote.
2- Kuweka rahani kwamba timu fulani au mchezaji fulani au mfano wa hivyo atashinda: Kwa hivyo, ikiwa timu yake itashinda, anashinda mali hizo. Na ikiwa timu yake itashindwa, basi anapoteza mali hizo.
3- Bahati nasibu na kadi za bahati nzuri: Hili ni kama vile kununua kadi kwa Dola kwa hivyo akawa amepata kuingia katika mchezo wa kuchukua kadi ya bahati nzuri. Kadi yake ikishinda, anapata zaidi ya thamani yake, sawa kiwe kichache alichopata au kingi.
4- Kushiriki katika mashindano kwa simu au kwa ujumbe wa rununu ambao umewekewa zaidi ya gharama zake za kawaida. Vile vile michezo yote inayofanywa kwa viungo vya mwili kama vile kukimbia, au michezo ya umeme na ya kielektroniki, au kupitia tovuti za mtandaoni, ambayo mchezaji huwa kati ya uwezekano mwili: kushinda mali au kuipoteza.