Sehemu ya sasa:
Somo Kuazima kitu
:idadi wanafunzi wengine walimaliza somo hili
Maana ya Al-'Aariya (kuazima)
Hukumu ya kuazima
Hekima ya sheria kuruhusu kuazima
Ni katika rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba ameruhusu kuazima; ili muazimwa aweze kukidhi haja zake, pamoja na muazima kupata ujira, kwa kumnufaisha ndugu yake kwa kitu ambacho bado ni chake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na saidianeni katika wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui." [Surat Al-Ma'idah: 2]
Imesimuliwa kutoka kwa Anas bin Malik – Mwenyezi Mungu amuwiye radhi – kuwa alisema: Siku moja, kulikuwa na hofu huko Madina, kwa hivyo, Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akaomba farasi aitwaye Al-Mandub kutoka Abu Twalha, na akamkwea. Aliporudi, akasema, "Hatukuona kitu chochote (cha kuogopesha), na hakika farasi huyu alikwenda kwa kasi kubwa." (Al-Bukhari 2627, Muslim 2307)
Masharti yanayofanya kuazima kuwa sahihi
Nguzo za kuazima kitu
Mtu aliyeazimwa anapaswa kuhifadhi kitu alichoazimwa, kukitunza, kukitumia kwa matumizi mazuri, akirudishe salama kwa mwenyewe. Kitu kilichoazimwa kikiharibika mikononi mwa muazimwa pasi na kukitumia, basi atadhaminika bila sharti lolote, sawia alipuuza au laa. Ama kikiharibika kwa matumizi yaliyoruhusika basi hakuna dhamana; isipokuwa ikiwa muazimwa akivuka mipaka au akipuuza, basi atakidhamini.
Yapaswa kwa aliyeazimwa arudishe kiazimwa ambacho alikiazima pindi amalizapo haja zake, na akirudishe salama kama alivyopewa, na hafai kukikatalia au kukikana, na akifanya hivyo basi ni haini, mwenye dhambi.
Muazima ana haki ya kutaka arejeshewe kiazimwa chake wakati wowote anaotaka bora muazimwa asidhuruke. Ikiwa katika kukirejesha kuna madhara kwa muazimwa, atachelewesha kukichukua mpaka yaondoke madhara hayo, kama vile aliyeazima shamba kisha muazimwa akapanda mimea humo, basi muazima haruhusiwa kuchukua shamba lake mpaka muazimwa avune.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:"Hakika Mwenyezi Mungu anawaamrisha mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapohukumu baina ya watu, mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayowaaidhi Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona." (An-Nisaa: 58)