Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Sunna za Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Dini ya Uislamu imetokana na vyanzo vikuu viwili; Qur-ani Tukufu na Sunnah za Mtume zilizotakaswa. Katika somo hili, utajifunza juu ya uhakika wa Sunnah ya Mtume na nafasi yake katika Uislamu.

  • Kujua fadhila za Sunna za Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
  • Kujua nafasi ya Sunnah katika kutunga sheria
  • Kuhisi ukuu wa kisheria wa Sunna.

Sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ni Ufunuo ambao Mwenyezi Mungu alimfunulia Nabii wake Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Nazo pamoja na Kitabu cha Mwenyezi Mungu kitukufu, ndio msingi na chanzo cha dini ya Uislamu. Na mbili hizi hazitengani kamwe kama vile kushuhudia kwamba hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kushuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu havitengani. Na yeyote asiyeamini Sunna, basi pia haamini Qur-ani.

Maana ya Sunnah

Sunnah ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ni maneno ya Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, vitendo vyake, masuala aliyoidhinisha bila yeye mwenyewe kuyafanya, sifa zake za kimaumbile na kimaadili.

Hadhi ya Sunna za Mtume

Sunnah za Mtume zina nafasi kubwa katika Uislamu. Na yanayoonyesha hayo ni kama yafuatavyo:

1. Ni chanzo cha pili cha sheria

Sunnah ni chanzo cha pili cha dini baada ya Qur-ani Tukufu. Imesimuliwa kutoka kwa Al-Muqaddam bin Ma'di Karb Al-Kindii kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: “Sikilizeni! Hakika mimi nilipewa Kitabu na mfano wake pamoja nacho. Sikilizeni! Hakika mimi nilipewa Qur-ani na mfano wake pamoja nayo. Sikilizeni! Amekaribia mno mtu kukaa kwenye kiti chake huku ameshiba na aseme: Shikamaneni na Qur-ani. Mtakachopata humo cha halali, kihalalisheni, na mtakachopata humo cha haramu, kiharamisheni." (Musnad Ahmad 17174)

2. Ni ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu

Sunnah ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ni ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Mwenyezi Mungu amesema: "Wala hatamki kwa matamanio." [Al-Najm: 3-5]

3. Ni kauli ya Qur-ani

Ndani ya Sunna ya Nabii kuna maelezo ya Qur-ani. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao, wapate kufikiri." (An-Nahl: 44)

Na Aya mbalimbali za Qur-ani Tukufu zilikuja katika hukumu za jumla katika masuala mengi. Kwa hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akazifafanua hukumu hizo kwa maneno yake au kwa kuzitekeleza kivitendo. Kwa mfano katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na mtiini Mtume, ili mpate kurehemewa." (An-Nur: 56)

Kuhifadhi kwa Mwenyezi Mungu Sunna ya Mtume

Sunna ya Nabii ni katika ukumbusho ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuhifadhi. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Hakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda." (Al-Hijr: 9) Na ukumbusho ni neno linalojumuisha mambo yote ambayo Mwenyezi Mungu alimfunulia Nabii wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kama vile Qur-ani na Sunna.

Miongoni mwa yenye kuonyesha kwamba Mwenyezi Mungu aliuhifadhi ukumbusho wake ni kwamba aliandalia Sunna za Nabii. Wanazuoni walifanya juhudi kubwa kukusanya Sunna na kuiandika, na kuiwekea kanuni zinazodhibiti usimulizi wake. Na wakatofautisha uongo, udanganyifu na makosa yaliyoingia ndani yake, na wakalidhibiti hilo vyema sana, na wakaihifadhi vyema sana, na pia wakadhibiti hali za wasimulizi wake.

Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu alichukua jukumu la kuihifadhi Sunnah kupitia hawa wasimulizi na wanazuoni ambao aliwatumia kuihifadhi Sunnah ya Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Kutumia Sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kama hoja

Sunna ya Nabii ni chanzo cha pili cha sheria baada ya Qur-ani Tukufu, na dini ya Mwenyezi Mungu haikamiliki isipokuwa kwa kufuata Kitabu na Sunna bega kwa bega.

Kwa hivyo, Sunnah ni chanzo muhimu katika kudhibiti hukumu za kisheria, na ni lazima kuzifanyia kazi, katika masuala ya kiimani na hukumu za kisheria.

Sunnah inawezakuja ili kuelezea hukumu za Qur-ani Tukufu, na pia huja kivyake katika kutunga hukumu mbalimbali. Hivyo basi ni kama Qur-ani katika kuhalalisha halali, na kuharamisha haramu.

Kuna ushahidi kutoka katika Qur-ani Tukufu na Hadithi za Mtume unaothibitisha kwamba sunna ni hoja, na pia ukiashiria hadhi yake katika kutunga sheria ya Kiislamu. Zipo Aya nyingi na Hadithi nyingi zinazoamrisha kushikamana na Sunnah, kuihitajia, na uwajibu wa kutii Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu." [Al-Hashr: 7]

Imesimuliwa kutoka kwa al-Maqdam bin Ma'd Yaqrib Al-Kindi, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Mtu yuko karibu sana kuegemea juu ya kochi lake, akizungumza juu ya hadithi miongoni mwa hadithi zangu, akasema: Kati yetu na nyinyi kuna Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo, kile tutakachokikuta ndani yake kwamba ni halali, basi sisi tunakihalalisha, na kile tunachokikuta ndani yake kwamba kimeharamishwa, basi tunakiharamisha. (Ibn Majah 12)

Kufuata Sunna

Mwenyezi Mungu aliwawajibishia waja wake kumtii Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kufuata Sunnah yake katika maneno, matendo na hali zake zote. Akasema: "Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu." [Al-Imran: 31] Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka.” (Al-A'raf :158)

Imesimuliwa kutoka kwa Al-Irbadh bin Sariya, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: "Basi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za makhalifa waongofu wanyoofu, na mzikamate na kuzing'ata kwa magego. Na jihadharisheni na mambo mapya, kwani kila jambo jipya ni uzushi na kila uzushi ni upotovu." (Abu Dawud 4607)

Kufuata kushikamana na kile ambacho Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema au kufanya, na kufuata mwendo wa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na njia katika kufuata amri zake na kujiepusha makatazo yake, na kuitekeleza dini na kuifanyia kazi.

Kufuata ni wajibu katika mambo ya wajibu na ni jambo linalopendekezwa katika mambo yanayopendekezwa.

Ubora wa kufuata Sunnah

Kufuata Sunnah kuna fadhila na matunda mengi, kama vile:

Katika kufuata Sunnah na kushikamana nazo kuna kujiepusha kufuata migawanyiko ambayo Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aliwaahidi watu hao adhabu ya moto. Imesimuliwa kutoka kwa 'Abdullah bin 'Amr, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Hakika Umma wangu utajiwa na yale yaliyowajia Banu Israili kama vile hatua za ndara zinavyofuatana kiasi kwamba kama mmoja wao alimuingilia mama yake hadharani, basi pia katika umma wangu kungekuwa na mwenye kufanya hivyo. Na hakika Banu Israili waligawanyika katika madhehebu sabini na mbili, nao Umma wangu utagawanywa katika madhehebu sabini na tatu, yote yataingia katika moto isipokuwa dhehebu moja tu." Wakasema: Na ni lipi hilo, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Akasema: "Ni yale ambayo mimi na maswahaba zangu tunafanya." (Tirmidhi 2641)

Katika kushikamana na Sunnah, kuna kufikia uongofu na usalama kutokana na kupotea. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka." (Al-A'raf :158) Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Hakika mimi nimewacha miongoni mwenu mambo mawili ambayo hamtapotea baada yake: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah yangu." (Mustadrak, cha Al-Hakim, 319)

Kukubaliwa kwa matendo mema kunategemea kuafikiana kwa matendo hayo na Sunnah, kwani ni lazima matendo ambayo mja anafanya yaafikiane na Sunnah ya Mtume. Imesimuliwa kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Yeyote anayefanya matendo ambayo sikuamrisha, basi yatakataliwa.” (Muslim 1718)

Katika kufuata Sunnah kuna kujinasibisha na Nabii,rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na mwenye kujitenga na Sunnah ni kujiweka mbali na Nabii. Imesimuliwa kutoka kwa Anas bin Malik, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa akasema: Kundi la watu watatu walikwenda kwa nyumba za wake wa Mtume,Rehema na amani za Allah zimshukie,wakiuliza jinsi Mtume,Rehema na amani za Allah zimshukie, alivyokuwa akifanya ibaada. Walipoambiwa, basi ni kana kwamba waliziona kuwa hazitoshi, na wakasema, "Sisi ni akina nani tukilinganishwa na Mtume, rehema na amani za Allah zimshukie? Na ilhali dhambi zake za zamani na za baadaye zimekwisha samehewa?" Kisha mmoja wao akasema, "Ama mimi, basi nitakuwa nikiswali usiku kucha abadani." Naye mwengine akasema, "Mimi nitakuwa nikifunga mwaka wote na wala sitafungua kamwe." Naye wa tatu alisema, "Mimi nitakaa kando na wanawake, na wala sitaoa abadani." Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwajia na akasema, "Nyinyi ndio wale mliosema hivi na vile? Ama wallahi! (kwa jina la Mwenyezi Mungu) Hakika mimi bila ya shaka ndiye mchamungu wenu nyote, lakini mimi hufunga saumu na ninafungua, na ninaswali na ninalala, na ninawaoa wanawake. Kwa hivyo, mwenye kukataa sunna (mwenendo) yangu, basi yeye si miongoni mwangu."

Na katika kushikamana na Sunna kuna kuokoka kutokana na majaribio na adhabu ya kudumu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Basi, na watahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu." [An-Nur: 63]

Katika kufuata Sunnah na kushikana nazo kuna kufuzu kupata furaha katika nyumba hizi mbili. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamwogopa Mwenyezi Mungu na wakamcha, basi hao ndio wenye kufuzu." (An-Nur: 52)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani