Sehemu ya sasa:
Somo Namna Muislamu anavyoamiliana na majanga
Tunaamini katika mipangilio ya Mwenyezi Mungu; mizuri na mibaya. Kwani hilo ni moja ya nguzo za imani. Na yote yanayowasibu waja miongoni mwa majanga ya magonjwa, maradhi ya kawaida na misiba, basi ni kwa sababu ya mipangilio ya Mwenyezi Mungu na kadari yake. Kwa hivyo ni lazima turidhie mipangilio yake na wala tusikasirike na kulalamika na kuhuzunika. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi kila kitu." (At-Taghabun: 11)
Muumini anaamini kwamba magonjwa hayaambuki kwa nguvu zake yenyewe, bali ni kwa amri na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Lakini pamoja na hayo, ametuamuru tufanye visababishi vya kihisia vya kiafya na vyenye kinga, kwa kujiepusha na visababishi vya maradhi na maeneo yaliyoambukizwa, na kuchukua tahadhari kwa kuacha kuchanganyika na wagonjwa. Amesema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakuna kuambukizana kwa ugonjwa bila amri ya Mwenyezi Mungu ('Adwaa), wala hakuna mkosi unaoweza kusababishwa tu na ndege (Twiyara), wala hakuna mkosi unaosababishwa na bundi (Hamah)," wala hakuna chochote kibaya katika mwezi wa Swafar. Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyokimbia kutoka kwa simba." (Al-Bukhari 5707)
Magonjwa ya milipuko ni adhabu ya haraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa makafiri na wanafiki, na ni rehema kwa waumini, ili kuwapandisha daraja zao na kufuta dhambi zao. Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimwambia 'Aisha Mwenyezi Mungu amridhie, alipomuuliza kuhusu tauni. "Ni adhabu iliyotumwa na Mwenyezi Mungu kwa yeyote yule amtakaye, na kwamba Mwenyezi Mungu aliifanya (hiyo tauni) kuwa rehema kwa Waumini, kwa kuwa hakuna yeyote ambaye janga la tauni litaenea katika nchi, kisha akakaa huko hali ya kuwa ana subira na matarajio ya malipo ya Mwenyezi Mungu, na akiamini kwamba hamna chochote kitakachompata isipokuwa kile ambacho Mwenyezi Mungu alimwandikia. Basi atapata malipo kama ya mtu aliyeuawa katika njia ya Mwenyezi Mungu." (Al-Bukhari 3474)
Inamlazimu Muislamu katika hali hizi, kuitikia nasaha za sekta rasmi, na achukue jukumu la kutanguliza masilahi ya umma juu ya masilahi ya mtu binafsi, na kushirikiana kwa kufanya mambo yenye kuhakikisha utulivu na maisha kurudi katika hali ya kawaida. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na saidianeni katika wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui." (Al-Maidah: 2)
Mambo yaliyoharamishwa wakati wa magonjwa ya milipuko
Hakuna shaka kwamba kueneza uvumi ni katika uongo ulioharamishwa, na pia husababisha hofu kati ya watu. Kwa hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari kutosambaza habari yoyote isiyo na uhakika. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika kutaja sifa za wanafiki: "Na linapowafikia jambo lolote lililohusu amani au la kitisho, wao hulitangaza. Na lau kuwa wangelipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanaochunguza, wangelijua." (An-Nisa: 83)
Uislamu umeharamisha kuhodhi bidhaa, kulaghai, kupandisha bei na kuchezea vyakula rahisi vya watu, haswa wakati wa majanga. Hili ni katika kula mali kwa batili, hiana, kupoteza amana, na kuwa na nafsi duni sana. Amesema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Mwenye kuhodhi chochote huku akitaka kuwapandishia bei Waislamu katika kitu hicho, basi yeye ni mwenye dhambi." (Al-Musnad 8617)
Kusambaza maambukizi kwa makusudi kutoka kwa mgonjwa mmoja kwenda kwa mtu mwenye afya njema kwa njia yoyote ile ni katika tendo lililoharamishwa la kukusudia kufanya jambo la haramu. Na hilo linachukuliwa kuwa miongoni mwa madhambi na makosa makubwa, na pia linasababisha adhabu ya kidunia. Adhabu hii inatofautiana kulingana na uzito wa tendo na athari zake kwa watu binafsi na athari zake kwa jamii.
Adhabu ya mwenye kusambaza maambukizi kwa makusudi kwa wengine:
4. Kutukana ugonjwa:
Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikataza kutukana homa. Imesimuliwa kutoka kwa Jabir bin Abdullah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimwambia Umma Saaib: "Usiitukane homa. Kwa maana, kwa hakika, hiyo huondoa madhambi ya wanadamu kama vile viriba vya kupulizia tanuru vinavyoondoa uchafu wa chuma." (Muslim 2575)