Sehemu ya sasa:
Somo Zawadi
:idadi wanafunzi wengine walimaliza somo hili
Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu Mtukufu, ni mkarimu na anapenda kutoa kwa wingi na ukarimu. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu, alikuwa mkarimu wa watu wote, na alikuwa akikubali zawadi na analipa juu yake, na anaitia kuikubali, na anahimiza juu yake. Na kutoa kulikuwa katika mambo yanayopendeza zaidi kwake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie.
Ni kummilikisha mtu kitu papo hapo bila malipo.
Na kauli yetu: "Kumilikisha" inaashiria kwamba mkataba wa zawadi ni katika mikataba ya kumilikisha.
Na maana ya "kitu" ni kitu chochote. Na vinaingia ndani yake vitu kama vile mali na visivyokuwa mali.
Na neno "kumilikisha kitu" liliondoa "kutoa zawadi ya manufaa" kwa sababu mbili:
Pia kitu kingine kilichotoka kwa kuali "kumilikisha" ni kumuondolea mtu deni, hata ikiwa ni kwa lafudhi ya zawadi. Kwa sababu kumuondolea mtu deni kunazingatiwa kwamba ni kuliangusha.
Hiba pia huitwa hadiyya (zawadi) au 'Atwiyya (kipawa) na hayo yote yanaingia katika mlango wa kufanya wema, hisani, kuunga uhusiano na kufanya mazuri.
Hukumu ya kutoa zawadi
Sheria ilihimiza kutoa zawadi kwa sababu ndani yake kuna kusafisha nafsi kutokana na uchafu wa ubahili, uchoyo, tamaa, na kwa sababu ya yale yaliyo ndani yake ya kuunga mioyo, kuimarisha msingi wa upendo kati ya watu, haswa ikiwa ni kwa jamaa wa mtu, jirani au adui. Ugomvi unaweza kutokea, na kujitenga na kupeana mgongo, na ukakatwa uhusiano wa jamaa, kisha zawadi ikaja na ikasafisha mioyo na kuondoa kila kitu kinachosababisha mgawanyiko kati ya watu. Mwenye kutoa kitu kama zawadi kwa ajili ya kuutafuta uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, atapata malipo na thawabu.
Imesimuliwa kutoka kwa 'Aaisha - Mwenyezi Mungu awe radhi naye - kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - alikuwa akipokea zawadi na akilipa juu yake. (Al-Bukhari, 2585)
Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Abbas - Mwenyezi Mungu awe radhi naye - kuwa alisema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alikuwa mkarimu zaidi wa watu wote. Na alikuwa mkarimu zaidi katika Ramadhani wakati Jibril anapokutana naye. Na alikutana naye kila usiku wa Ramadhani, na anamsomesha Qur-ani. Kwa hivyo, Mtume wa Allah - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - anakuwa mkarimu zaidi wa heri hata kuliko upepo ulioachiliwa." (Al-Bukhari 6, na Muslim 2308)
Nguzo za zawadi
Masharti ya zawadi
Wanazuoni walitofautiana kuhusiana na sharti la kwamba ni lazima zawadi iwe inajulikana. Na pia katika sharti la kwamba ni lazima iwe imegawanywa, na siyo imejumuishwa na kuenea katika vitu vingine.
Mwenye kumpa zawadi afisa msimamizi, au mfanyakazi, au wengineo kwa ajili ya kupata masilahi fulani ambayo hana haki nayo, basi hilo linakuwa haramu kwa mtoa zawadi na anayepewa zawadi. Kwa sababu hiyo ni rushwa ambayo amelaaniwa mwenye kuichukua na mwenye kuitoa.
Ikiwa ataitoa kama zawadi ili kujizuilia udhalimu fulani, au ili apewe haki yake ya wajibu, basi zawadi hii ni haramu kwa anayeikuchukua, lakini inaruhusiwa kwa mtoaji ili kuhifadhi haki yake na kuuzuia uovu wa huyo anayeichukua.
Imesimuliwa na Abu Humaid As-Saidi, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kuwa alisema: Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimtumia mwanamume fulani kutoka kwa Banu Asad, aitwaye Ibnul Utbiyyah, kwa ajili ya kukusanya sadaka. Aliporudi, akasema: Hii ni yenu, na hii yangu, nimepewa kama zawadi. Kwa hivyo, Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasimama juu ya mimbari, akamhimidi na kumsifu Mwenyezi Mungu, kisha akasema, "Ana nini mfanyakazi tunayemtuma, kisha anakuja na kusema, 'Hii ni yako, na hii ni yangu. Kwa nini hakukaa katika nyumba ya baba yake na mama yake, kisha akaona kama atapewa zawadi au la. Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, hatachukua chochote kwayo isipokuwa atakuja nayo Siku ya Qiyama akiibeba shingoni kwake. Ikiwa ni ngamia, atakuwa analia kwa sauti ya ngamia, au ng'ombe akilia kwa sauti ya ng'ombe, au kondoo kwa sauti ya kondoo." Kisha akainua mikono yake hadi tukaona weupe wa kwapa zake. "Je, nimefikisha?" mara tatu. (Al-Bukhari 7174, na Muslim 1832) Khuwaar ni sauti ya ng'ombe. Rugha ni sauti ya ngamia. Ghura ni weupe uliochanganyika na kahawia. Ta'iar ni kulia kwa sauti kubwa sana.